Wednesday, May 11, 2016

UCHUKUZI SC VINARA MEI MOSI WABEBA VIKOMBE 11


Wachezaji wa Uchukuzi SC wakiwa wamevipanga vikombe 11 walivyotwaa kwenye michezo mbalimbali ya Mei Mosi, iliyomalizika juzi mkoani Dodoma


TIMU ya Uchukuzi SC iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, imeibuka kinara kwenye mashindano ya Mei Mosi baada ya kutwaa vikombe 11 vya michezo mbalimbali. Timu hiyo inajumuisha wanamichezo kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

Timu hiyo imetwaa ubingwa katika michezo ya netiboli, baiskeli na bao  (wanaume), kamba (wanawake na wanaume); huku vikombe vya ushindi wa pili ni vya michezo ya bao (wanawake) na draft (wanaume); wakati vya ushindi wa tatu  ni katika soka, karata (wanaume), riadha (wanawake na wanaume).

Hata hivyo, kutokana na uwingi wa vikombe timu hiyo ilitangazwa  mshindi wa jumla  kwenye sherehe za Mei Mosi na kukabidhiwa kombe na Mh. Rais John Magufuli.

Timu nyingine na idadi ya vikombe zilizopata ni TAMISEMI saba kikiwemo cha ubingwa wa soka baada ya kuwafunga GGM katika fainali kwa magoli 2-0, huku TPDC wakiwa na vikombe vitano sawa na Tanesco.Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wamejikusanyia vikombe vinne, Ujenzi vikombe viwili, na Mawasiliano, Ukaguzi  na Halmashauri ya Nyasa kila mmoja wana kikombe kimoja kila mmoja.

Awali katika michezo iliyochezwa jana timu ya Uchukuzi SC iliwafunga Tamisemi kwa magoli 18-15 katika mchezo wa netiboli, ambapo wafungaji wake Tatu Kitula na Matalena Mhagama waliwapeleka puta wapinzani wao na hadi mapumziko walikuwa mbele kwa magoli 11-7.

Washindi wote walikabidhiwa kombe na mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU), Mussa Kalala, ambaye  katika hotuba yake aliwashutumu viongozi walioshindwa kupeleka timu zao kwenye mashindano hayo na kusema michezo mahala pa kazi husaidia kuijenga miili ya wafanyakazi kuendelea kuwa mikakamavu na kuwa na afya bora, ambapo hutoa huduma bora iliyotukuka na kuzalisha tija zaidi.




No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...