Wednesday, April 22, 2015

TMA YAJIKITA KATIKA KUKIDHI MATAKWA YA WADAU WA SEKTA MBALIMBALI

Mkurugenzi wa utafiti na matuzi wa TMA Dkt. Ladislaus Chang'a akimkaribisha mkurugenzi mkuu Dkt. Agnes Kijazi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa warsha ya wataalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali vya TMA waliokutana ili kufanyia kazi maoni ya wadau wa sekta za kilimo, afya, maji, na nishati katika ukumbi wa hoteli ya Bluepearl, Dar es Salaam tarehe 21 Aprili 2015.
Mgeni rasmi Dkt. Kijazi akiongea na wana warsha katika ufunguzi wa warsha ya wataalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali vya TMA waliokutana ili kufanyia kazi maoni ya wadau wa sekta za kilimo, afya, maji, na nishati katika ukumbi wa hoteli ya Bluepearl, Dar es Salaam tarehe 21 Aprili 2015.

Wanawarsha wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa warsha ya wataalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali vya TMA waliokutana ili kufanyia kazi maoni ya wadau wa sekta za kilimo, afya, maji, na nishati katika ukumbi wa hoteli ya Bluepearl, Dar es Salaam tarehe 21 Aprili 2015.
Mkurugenzi mkuu na wakurugenzi wa divisheni sambamba na wanawarsha wengine wakifuatilia mada mbalimbali zilizotolewa na watoa mada (pichani hapo juu)
Mgeni rasmi akifunga warsha ya siku moja ya wataalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali vya TMA waliokutana ili kufanyia kazi maoni ya wadau wa sekta za kilimo, afya, maji, na nishati katika ukumbi wa hoteli ya Bluepearl, Dar es Salaam tarehe 21 Aprili 2015.
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na wanawarsha  wa warsha ya wataalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali vya TMA waliokutana ili kufanyia kazi maoni ya wadau wa sekta za kilimo, afya, maji, na nishati katika ukumbi wa hoteli ya Bluepearl, Dar es Salaam tarehe 21 Aprili 2015. 



Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imeendelea na mkakati wake wa kuhakikisha wadau wa sekta mbalimbali nchini wananufaika na huduma za hali ya hewa katika shughuli zao za kila siku. Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes kijazi ambaye pia alikuwa mgeni rasmi alielezea umuhimu wa mkakati huo wakati akifungua mkutano wa wataalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali vya TMA waliokutana ili kufanyia kazi maoni ya wadau wa sekta za kilimo, afya, maji, na nishati katika ukumbi wa hoteli ya Bluepearl, Dar es Salaam tarehe 21 Aprili 2015.

‘TMA kwa kipindi cha miaka ya hivi karibu imekuwa ikikutana na wadau wa sekta mbalimbali na kupata maoni yao juu ya huduma zinazotolewa (user engagement) na vilevile kubadilisha namna ya uhifadhi wa takwimu za hali ya hewa (data rescue and digitization), kwa kupitia maoni hayo Mamlaka imeona ni wakati muafaka kuwakutanisha wataalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali ili kujadili na kupata suluhisho la kuboresha huduma zetu’, alisema Dkt. Kijazi.

Mamlaka imekuwa ikishirikiana na taasisi za kitaifa na kimataifa ili kuhakikisha utoaji wa huduma zake unakidhi matakwa ya wadau. Katika kutimiza hilo tarehe 11 Novemba 2014 TMA ilisaini makubaliano ya kushirikiana katika kutelekeza baadhi majukumu yake na Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza ambapo mambo makuu yalikuwa ni kuhakikisha watumiaji wa huduma za hali ya hewa nchini wanaridhika na huduma zitolewazo na vilevile kuboresha mfumo wa kuhifadhi takwimu za hali ya hewa.

Katika mkutano huu ambao umewahusisha pia wakuu wa kanda kutoka TMA na wasimamizi wa vituo vya hali ya hewa-kilimo vinavyoendeshwa na Mamlaka vilivyopo nchini,washiriki watapata fursa ya kujadili na kutolea maamuzi maoni ya wadau wa sekta ya kilimo, nishati, maji, afya na habari na pia kujipanga katika kuwafikia wadau wengine.

IMETOLEWA NA MONICA MUTONI, OFISI YA UHUSIANO TMA





No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...