Thursday, September 4, 2014

MWELEKEO WA MVUA KWA KIPINDI CHA OKTOBA - DISEMBA 2014 NCHINI


Dondoo muhimu kwa ufupi:

Taarifa hii inatoa tathmini ya mvua za masika (Machi - Mei) 2014 na mwelekeo wa mifumo ya hali ya hewa na mvua kwa kipindi  cha mwezi Oktoba hadi Disemba, 2014(Vuli).


1. Mwelekeo wa mvua kwa kipindi cha Oktoba-Disemba, 2014 Vuli unaonyesha kuwa;
·        Hali ya mvua inatarajiwa kuwa ya  kuridhisha katika maeneo mengi ya       nchi hata hivyo mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa  katika baadhi ya maeneo ya kusini mwa nchi hususan mkoa wa Ruvuma.
·        Msimu huu mvua zinatarajiwa kuanza mapema mwezi Septemba katika maeneo ya ziwa Viktoria, nyanda za juu kaskazini mashariki na pwani ya kasikazini
 2. Athari na Ushauri
·        Mvua za kutosha zinatarajiwa kwa shughuli za  kilimo katika maeneo mengi ya nchi.
·        Vina vya maji katika mito na mabwawa vinatarajiwa kuongezeka katika maeneo mengi ya nchi.
·        Maji yatumike kwa uangalifu na kuzingatia taratibu za uvunaji, uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali maji
·        Matukio ya migogoro inayosababishwa na mifugo, wanyamapori na shughuli za binadamu na kilimo hayatarajiwi kujitokeza kwa kiasi kikubwa.
·        Vipindi vya mvua kubwa vinaweza kuongeza matukio ya mafuriko na uharibifu wa mali na miundombinu.
·        Milipuko ya magonjwa yanayosababishwa  na kutuama kwa maji na utiririshaji wa majitaka usiodhibitiwa inaweza kujitokeza.
·        Hatua stahiki katika utunzaji wa mazingira, upatikanaji wa maji safi na salama, na usambazaji wa madawa, maji na chakula ikiwa ni hatua za kujiandaa na kukabiliana na majanga yanayoweza kutokea


Imetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania





No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...