Thursday, August 21, 2014

KAMATI YA TAIFA YA MAAFA (TANDREC) YAKUTANA KUZUNGUMZIA UTEKELEZAJI WA MPANGO MAALUM WA KIMATAIFA WA KUHAKIKISHA HUDUMA ZA HALI YA HEWA ZINAWAFIKIA JAMII ZIKIWA NA UBORA HASA KWA NCHI ZINAZOENDELEA (GFCS) KATIKA NGAZI YA KITAIFA.



Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt Florence Turuku (wa tatu kutoka kushoto), Mwakilishi wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Mashariki na Kusini mwa Afrika (wanne kutoka kushoto) Dkt Ellijah Mkhala, na  Dkt. Agnes Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TMA (wa pili kutoka kushoto) katika picha ya pamoja kwenye kikao cha Kamati ya Taifa ya Maafa (TANDREC) kilichofanyika tarehe 14 Agosti 2014.




Mamlaka ya Hali ya Hewa  kwa kushirikiana  na Shirika la Hali ya Hewa Duniani na Ofisi ya Waziri Mkuu waliandaa kikao cha Kamati ya Maafa ya Taifa (TANDREC) kuzungumzia utekelezaji wa GFCS hapa nchini. Mwenyekiti wa kikao hicho ni  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florence Turuku ambapo majadiliano yalijikita zaidi katika kuhakikisha ushirikiano kati ya Kitengo cha Maafa nchini na GFCS. Kikao pia kiliweza kupitia mapendekezo muhimu mawili; kwanza, Jukwaa la Kitaifa la Wadau wa Maafa kuendelea kutumika katika kubadilishana mawazo na watumiaji na watoaji wa huduma za hali ya hewa nchini. The meeting adopted two important recommendations;  Pili, TANDREC itumike kama kamati ya maendeleo ya GFCS.
Aidha, katika hotuba ya ufunguzi Dkt Turuku alielezea umuhimu wa utekelezaji wa GFCS na kazi za kamati ya Taifa kusimamia maendeleo ya GFCS nchini.
                                                                                                          
Dkt. Ellijah Mukhala, Mwakilishi wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Mashariki na Kusini mwa Afrika, alielezea kwa kifupi nia ya utekelezaji wa GFCS, ambao kwa hivi sasa umeanza kufanya kazi kwa nchi za Tanzania na Malawi kwa udhamini wa Seriakali ya Norway. Alielezea furaha yake kwa utekelezwaji wa GFCS kwa Tanzania mpaka hivi sasa imeundwa Timu ya Mradi inayoongozwa na TMA, na mkutano wa wadau wa hali ya hewa uliojumuisha zaidi ya wadau 60 kutoka kwa taaisi za serikali,taasisi zisizo za kiserikali, wanahabari, katika mkutano huu mapendekezo mbalimbali yalitolewa yenye lengo la kuboresha huduma za hali ya hewa nchini.
 IMETOLEWA NA  : MONICA MUTONI, OFISI YA UHUSIANO TMA


No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...