Wednesday, July 2, 2014

MWELEKEO WA HALI YA JOTO NA MVUA KATIKA KIPINDI CHA JUNI HADI AGOSTI 2014


Taarifa hii inatoa mwelekeo wa mifumo ya hali ya hewa, joto na mvua katika kipindi cha miezi ya Juni hadi Agosti (JJA) 2014.

1.         MIFUMO YA HALI YA HEWA

Mifumo ya hali ya hewa inaonesha uwezekano wa kuongezeka kwa joto la bahari katika eneo la ukanda wa Tropiki la bahari ya Pasfiki kwa kipindi cha miezi ya Juni hadi Agosti 2014. Ongezeko kidogo la joto linatarajiwa katika ukanda wa magharibi ya bahari ya Hindi. Aidha joto katika bahari ya Atlantik linatarajiwa kuwa chini ya wastani. Hali hiyo inatarajiwa kusababisha upepo kuvuma kutoka magharibi ukielekea mashariki katika maeneo mengi ya nchi. Joto la bahari la juu ya wastani linatarajiwa katika eneo la ncha ya kusini ya bara la Afrika hivyo kuathiri msukumo wa upepo wa kusi katika kipindi cha miezi ya  Juni hadi Agosti2014.   Hali hii inatarajiwa kusababisha hali ya baridi katika kipindi hicho. Aidha, vipindi vifupi vya mvua za vinatarajiwa katika maeneo machache ya ukanda wa Ziwa Viktoria, ukanda wa pwani na katika maeneo ya miinuko.


2: VIWANGO VYA CHINI VYA JOTO NA MVUA: JUNI HADI AGOSTI, 2014

2.1 MATARAJIO YA VIWANGO VYA CHINI VYA JOTO KWA MIEZI YA JUNI HADI AGOSTI 2014
Kindi cha mwezi Juni hadi Agosti, maeneo mengi ya nchi yanarajiwa kuwa makavu na yenye hali ya baridi katika majira haya ya kipupwe. Mifumo ya hali ya hewa inaonesha kuwa na hali ya joto la wastani katika kipindi cha miezi ya Juni hadi Agosti 2014 katika maeneo mengi. Aidha, izigatiwe kuwa hali ya baridi inatarajiwa zaidi nyakati za usiku hadi mapema asubuhi. Matarajio ya viwango vya chini vya joto katika kipindi hicho ni kama ifuatavyo:
Ukanda wa ziwa Victoria (Mikoa ya Mwanza, Mara, Chato, Kagera, Shinyanga na Simiyu)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa juu ya wastani(Juu ya nyuzi joto 17.2 0C)  katika maeneo mengi. Hata hivyo, katika maeneo ya kusini ya mikoa ya Shinyanga na Simiyu hali ya joto inatarjiwa kuwa chini ya wastani.
Ukanda wa pwani ya kaskazini (Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, maeneo ya kaskazini ya mkoa wa Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa juu ya wastani(Juu ya nyuzi joto 22.9 0C) katika maeneo mengi. Hata hivyo, katika maeneo ya miinuko ya mkoa wa Tanga hali ya joto inatarajiwa kuwa chini ya wastani(Chini ya nyuzi joto 15.9 0C).

Ukanda wa nyanda za juu kaskazini mashariki (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa ya wastani(Kati ya nyuzi joto 13.0 0C na 15.8 0C)  katika maeneo mengi. Hata hivyo, katika maeneo ya miinuko viwango vya joto vinatarajiwa kuwa chini ya wastani(Chini ya nyuzi joto 13.0 0C).
Ukanda wa magharibi (Mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa ya wastani(Kati ya nyuzi joto 14.9 0C na17.0 0C) katika maeneo mengi. Hata hivyo, katika maeneo ya kaskazini ya mkoa wa Kigoma (Kibondo) hali ya joto inatarajiwa kuwa ya wastani(Juu ya nyuzi joto 17.0 0C).

Ukanda wa kati (Mikoa ya Singida na Dodoma)
Hali ya  joto inatarajiwa kuwa ya wastani(Kati ya nyuzi joto14.1 0C na 14.7 0C ) katika maeneo mengi. Hata hivyo, vipindi vya upepo mkali wenye kuambatana na baridi vinatajiwa katika maeneo hayo.
Ukanda wa pwani ya kusini  (Mikoa ya Mtwara na Lindi)
Hali ya  joto inatarajiwa kuwa juu ya wastani(Juu ya nyuzi joto 19.10C)  katika maeneo mengi.
  Ukanda wa kusini  (Mkoa wa Ruvuma)
Hali ya  joto inatarajiwa kuwa chini ya wastani(Chini ya nyuzi joto 11.80C) hususan maeneo ya magharibi mwa mkoa wa Ruvuma(Songea na mwambao wa Ziwa Nyasa). (Aidha, viwango vya joto la wastani vinatarajiwa kwa maeneo mengine ya ukanda wa kusini.)
Ukanda wa nyanda za juu kusini-magharibi (Mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe pamoja na maeneo ya kusini ya mkoa wa Morogoro)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa ya baridi kali ambapo viwango vya joto vinatarajiwa kuwa  chini ya wastani(Chini ya nyuzi joto 6.00C). Hata hivyo, katika maeneo ya kaskazini ya mkoa wa Iringa hali ya joto inatarajiwa kuwa ya wastani. 

2.2  MWELEKEO WA MVUA KWA KIPINDI CHA JUNI HADI AGOSTI 2014

Kipindi cha mwezi Juni hadi Agosti kwa kawaida huwa ni kikavu kwa ujumla, hata hivyo vipindi vifupi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo ya ukanda wa ziwa Victoria, nyanda za juu kaskazini mashariki na pwani ya kaskazini .  Hivyo matarajio yake ni kama ifuatavyo:

Ukanda wa ziwa Victoria (Mikoa ya Mara na Kagera)
Vipindi vya mvua ya wastani vinatajiwa katika maeneo hayo, hususan miezi ya Julai na Agosti 2014

Ukanda wa pwani ya kaskazini (Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, maeneo ya kaskazini ya mkoa wa Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba)
Vipindi vya mvua za wastani vinatajiwa katika maeneo haya, hususan mwishoni mwa mwezi Juni na katika kipindi cha  miezi ya Julai na Agosti 2014

Ukanda wa nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara)
Vipindi vya mvua za wastani vinatajiwa katika maeneo hayo, hususan maeo yenye miinuko na katika miezi ya Julai na Agosti 2014.

3: ATHARI NA USHAURI
Katika kipindi hicho hali ya hewa inatarajiwa kuwa ya wastani katika maeneo mengi na vipindi vya baridi kali katika baadhi ya maeneo. Hivyo, kwa shughuli zinazotegemea hali ya joto wadau wanashauriwa kuchukua hatua stahiki ili kukabiliana na madhara yanayo weza kutokea kutokana hali ya hewa inayotarajiwa. Pamoja na utabiri huu wa muda mrefu, ni muhimu pia watumiaji wakazingatia taarifa za hali ya hewa zinazotolewa kwa vipindi vifupi.
Mamlaka inawashauri watumiaji wa taarifa za hali ya hewa waendelee kutafuta, kupata  na kufuata ushauri wa wataalamu  katika sekta husika.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania itaendelea kufuatilia mifumo ya hali ya hewa na kutoa mrejeo kila inapobidi.
 


    



No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...